MSANII nyota katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Belle9 amefunguka na kusema msanii nguli katika muziki wa Hip Hip nchini Afande Sele anafaa kuwa mbunge 2015.
Nyota huyo aliyabainisha hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Afande Sele amabaye tayari katangaza nia yake
ya kugombea katika Jimbo la Moroogoro Mjini
ifikapo mwaka 2015 amejikuta kupewa ufagio hilo na msanii Belle9.
"Ni mtu muhimu katika nafasi ya kuongoza jimbo
jamii kubwa huwa inamkubali anastahili
kugombea jimbo hilo,"alisema msanii huyo.
Belle9 pia alisema anawazimia pia baadhi ya wasanii wengine waliowahi kubamba na nyimbo zao kusumbua anga za muziki.
Pia msanii huyo alisema amejipanga kufikisha muziki kwenye 'levo' za kimataifa mwaka huu ambapo nchini Uganda yuko mbio kumshirikisha katika kazi zake za sanaa msanii Bebe Cool .
Comments