MIMBA
ya msanii wa hiphop hapa Bongo, Happy Peter maarufu kama Sister P,
imeyeyuka kufuatia mazoezi makali ya kujiandaa na wimbo wake mpya.
Akiongea
katika ofisi za Saluti5 jana jioni, Sister P aliyetamba enzi hizo na
kibao chake “Anakuja”, alisema anasikitika kuwa mimba yake imeharibika.
“Nilikuwa
nafanya mazoezi makali ya kukimbia ufukweni pamoja na kuingia gym ili
nipate stamina ya kupasuka vizuri kwenye ‘mic’ kumbe nilikuwa nauweka
rehani ujauzito wangu.
“Siku
moja baada ya kutoka mazoezini nikaenda studio kuingiza sauti, wakati
naendelea kufanya makamuzi nikapatwa na maumivu makali ya tumbo.
“Nikakimbizwa
hospitali na baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa mimba imeharibika”
alisema Sister P msanii msela kupindukia kiasi cha kufanya watu wapate
utata juu ya jinsia yake.
Sister P amesema wimbo wake mpya uliosababisha kupoteza ujauzito wake umeshakamilika na hivi punde atauachia hewani.
Hivi
karibuni gazeti moja liliandika juu ya ujauzito wa Sister P na kuzua
mshtuko mkubwa wengi wao wakiwa hawaamini kama msanii huyo ana bwana
achilia mbali kuwa na mimba.Chanzo:www.saluti5.com
Comments