SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za
makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe
Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba
hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama
wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro
wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF) ambalo linajengwa katika ti ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa
na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na
nyumba za kulala.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo
Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo
linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na
Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali
(kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni
kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua
zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani
katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF
Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika
zitauzwa kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu
wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment)
zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Comments