MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura
yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana
hasira.
Amesema, Rais Kikwete
hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au
serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya
kazi.
Mama Salma Kikwete ametoboa
siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua,
kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na
kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa
NEC.
"Siyo kweli kwamba Rais Jakaya
Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa
mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira, tena sana pale mtendaji au
mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe
katika kazi za Chama au serikali yake", alisema Mama Salma Kikwete.
Mama
Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya mshereheshaji mmoja kwenye mkutano
huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema
kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa kupindukia na kuuliza umati wa
wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kwamba je ni nani amewahi kumuona
amenuna.
"Natoa ofa kama hapa kuna
mtu aliyewahi kumuona mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono.
Akitokea ntampa sh. elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya kwanza, ya pili
unaona hakuna", alisema Muhsini.
Wakati
akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye mkutano huo alinyoosha mkono,
lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. "Aaa
wewe sikupi zawadi", alisema Muhsini lakini papo hapo akakatishwa na
Mama Mama Kikwete.
"Hata kama humpi
hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete
hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa
mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana hasira, tena sana pale mtendaji
au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya
kizembe..." alisema Mama Kikwete.Chanzo:mpekuziblog
Comments