WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya soka ya Kombe la Shirikisho,
Azam jana walianza vyema kampeni za kutwaa taji hilo baada ya kuichapa
Al Nasir Juba ya Sudan mabao 3-1 katika mechi ya awali iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Kipre Tchetche ndiye aliyeibuka shujaa wa Azam baada ya kuifungia mabao mawili katika muda wa dakika 10 za mwisho.
Abdi Kassim 'Babi' alikuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za wasudan dakika ya 14 baada ya kuunganisha wavuni kwa kichwa krosi kutoka kwa beki Malika Ndeule, aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi.
Wasudan walisawazisha dakika ya 38 kwa bao lililofungwa na Fabian Elias baada ya mabeki wa Azam kuzembe kuokoa mpira uliopigwa kwenye lango lao.
Azam ingeweza kutoka uwanjani na ushindi mkubwa wa mabao, lakini washambuliaji wake, Babi na Tchetche walikosa umakini.
Kuingia kwa John Bocco katika kipindi cha pili kuliongeza kasi ya mashambulizi kwa Azam kutokana na mshambuliaji huyo kuonyesha uchu mkubwa wa kufunga mabao.
Kutokana na ushindi huo, Azam sasa inahitaji sare ya aina yoyote timu hizo zitakaporudiana wiki mbili zijazo mjini Juba. Inatoka kwa mdau.

Comments