MWENYEKITI wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete anatembea na mkoba wenye majina ya wajumbe wapya wa Kamati Kuu (CC) ya CCM hadi hapo atakapowatangaza kesho kutwa hivyo kuwaacha wajumbe wengi wa Halmashauri Kuu (NEC) wa chama hicho wakiwa roho juu iwapo majina yao ni miongoni mwake au l
Baadhi ya wajumbe hao walionekana jana katika viunga vya ofisi za makao makuu ya chama hicho (White House) mjini hapa wakiomba kura kwa wajumbe wenzao kama majina yao yatakuwa kwenye orodha hiyo ya Rais Kikwete...
“Nawaombeni mnikumbuke jina langu
likija,” alisema mmoja wa wajumbe wa NEC ambaye pia ni Waziri wa
Serikali ya awamu ya nne ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za
kimaadili.
Ingawa baadhi ya wajumbe walimkejeli,
wapo waliomtia moyo wakimwambia: “wewe bwana una akili sana, umekifanyia
Chama kazi nyingi sana. Lazima jina lako lirudi.”
Wajumbe wa CC walipaswa kuteuliwa
kwenye NEC iliyofanyika Novemba 10 hadi 12, mwaka jana lakini Rais
Kikwete alisitisha mpango huo kwa kile alichosema kuwa anahitaji muda
zaidi ili awafahamu vyema wajumbe wa NEC mpya iliyoteuliwa wakati huo.
Hali hiyo imekuwa ikiwaweka roho juu
wajumbe wa NEC kwa kuwa wengi wao na hasa waliokuwa kwenye CC iliyopita
wanatamani kuteuliwa tena.
Kutokana na subira hiyo ya Rais
Kikwete, Chama hicho tawala kilisheherekea kutimiza umri wa miaka 36,
Jumanne iliyopita mjini Kigoma, bila ya kuwa na Kamati Kuu, ambayo
ilitakiwa kukaa na kutathmini mafanikio na matatizo ya chama hicho.
Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye alisema kuwa NEC itafanya kikao kwa siku mbili kuanzia
kesho kutwa chini ya Uenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Nnauye, pamoja na mambo
mengine kikao hicho kitatanguliwa na semina ya siku mbili kwa wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa.“
Lengo la semina hii ni kuwaongezea
wajumbe uelewa kuhusu masuala ya chama hicho na Serikali yake hasa
ikizingatiwa kwamba wengi wa wajumbe ni wapya kutokana na wengi
kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa chama mwaka jana,” alisema.
Nnauye alisema kuwa semina hiyo
itakuwa na mada kuu nne ambazo ni pamoja na ‘Nafasi ya wajibu wa mjumbe
wa Halmashauri Kuu Taifa’, ‘Umuhimu wa maadili kwa viongozi na watendaji
wa chama hicho’, ‘Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa
Taifa wa nane wa CCM’ pamoja na ‘Mkakati wa kukuza ajira nchini’.
“Semina hii itafuatiwa na Mkutano
rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine uchaguzi
wa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama,” aliongeza Nnauye.
Gazeti Mwananchi
Comments