Polisi watoa taarifa kamili za kuzama kwa Jahazi liitwalo Sunrise likitokea Tanga kulekea visiwani Zanzibar
millardayo.com
iliripoti kuhusu kuzama kwa Jahazi liitwalo Sunrise likitokea Tanga kulekea
visiwani Zanzibar likiwa na abiria 32 ambapo lilizama kwenye lile eneo la Nungwi
.
Polisi Zanzibar walisema “tayari tumeshapokea
watu 22 waliookolewa wakiwa wazima na hakuna maiti iliyopatikana mpaka sasa
hivi, waliokuwemo kwenye chombo ni watu 32 hivyo watu bado watu 10 hawajulikani
walipo”
Baada ya hapo millardayo.com iliahidiwa tena
kuongea na Polisi baadae ili kujua zoezi la uokoaji limefikia wapi, kweli Polisi
walitoa tamko lao usiku wakati AMPLIFAYA ya CLOUDS FM inamalizika.
Namkariri Kamanda akisema “Oparesheni
imemalizika na hakuna yeyote aliepatikana zaidi ya walewale 22 wa mwanzo ambao
walipelekwa hospitali na wote wamesharuhusiwa isipokua nahodha ambae bado
amelazwa hospitali kwa matibabu, kimsingi shauri linaendelea na upelelezi na
baada ya kukamilika sheria itachukua mkondo wake”
Kwa taarifa hiyo inamaana watu 10 ambao
hawakuokolewa mwanzoni wanahofiwa kufa maji manake mpaka oparesheni ya uokoaji
imemalizika hawakuonekana, kwa ushahidi unaweza kumsikiliza Kamanda wa polisi
akiongea hapo chini.
Chanzo: millardayo.com
Comments