HABARI/PICHA na bongostaz.blogspot.com BONDIA Mtanzania, Francis ‘SMG’ Cheka usiku wa kuamkia leo ametawazwa kuwa bingwa mpya wa dunia wa WBF, katika uzito wa Super Middle baada ya kumshinda Mmarekani, Phil Williams kwa pointi katika pambano la Raundi 12, lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Jaji wa kwanza Eddie Marshall kutoka Afrika Kusini alitoa pointi 116 kwa 115, jaji wa pili Fidel Hayness alitoa pointi 119 kwa 118 na jaji wa tatu, John Chagu alitoa pointi 117 kwa 116 (wote wa Tanzania), wakimpa ushindi Cheka. Kwa ushindi huo, Cheka amefuata nyayo za bondia mwingine Mtanzania, Rodgers ‘Tiger’ Mtagwa ambaye aliwapiga Wamarekani kadhaa kwao, ambako anaishi tangu 1998. Bondia Francis Cheka wa Tanzania akimtupia konde Mmarekani, Phil Williams katika pambano la Raundi 12 kuwania ubingwa wa dunia uzito wa Super Middle usiku huu ukumbi wa Diamond Jubilee kuwania taji la WBF. Cheka ameshinda kwa pointi . Thomas Mashali kulia ames...