Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
RASMI. Yanga SC imejitoa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, kwa sababu timu yao haina benchi la Ufundi, baada ya kufukuzwa kwa Kocha Mkuu, Ernie Brandts.
Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY muda huu kwamba, uongozi umefikia hatua hiyo kwa sababu bado hawajapata benchi jipya la Ufundi.

Yanga SC ilikuwa imepangwa Kundi C la
michuano hiyo inayoanza kesho pamoja na Spice Star, Azam FC na Tusker ya
Kenya- maana yake kwa kujitoa kwao, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA)
kitalazimika kupanga upya Ratiba yake au kuiingiza timu nyingine katika
nafasi ya mabingwa hao wa Bara.
Comments