Ndugu zangu,
Kwenye nchi ya Wasadikika kuna mambo mengi ya ajabu. Wasadikika kwa sasa wako kwenye 'hatari kubwa' ya kuzama kwenye mafuriko ya habari.
Kwenye nchi ya Wasadikika kuna mambo mengi ya ajabu. Wasadikika kwa sasa wako kwenye 'hatari kubwa' ya kuzama kwenye mafuriko ya habari.
Haijapata kutokea kwenye Nchi ya
Wasadikika kuuanza mwaka na mafuriko ya habari. Kwa sasa Nchi ya
Kusadikika ina habari nyingi kiasi cha wahariri kwenye vyumba vya habari
kufikiria kuongeza kurasa za magazeti. Na kwenye redio kuongeza dakika
za matangazo.
Na kawaida ya mafuriko huja na mazagazaga. Ndio, kwenye mafuriko haya ya habari kuna ' mazagazaga' ya habari pia.
Na Wasadikika wanapenda sana '
mazagazaga'. Ni zile habari zenye kuzagaa mitaani na mara nyingi huwa
hazina vichwa wala miguu. Na nyingine haziandikwi kabisa magazetini wala
kutangazwa redioni- Ni mazagazaga tu yenye kuzaa habari pia.
Ndio, mazagazaga ni habari zisizoumiza
sana vichwa, maana huna haja ya kifikiri sana na unaweza kuzianzia
katikati na hata mwisho wa habari na ukawa na cha kuzungumza. Naam,
Wasadikika wanapenda sana mambo ya kuambiwa na yanayotokana na
walichosema akina Sadiki.
Hata hivyo, kwenye nchi ya Wasadikika,
ukiachana na ' mazagazaga' yanayoelea na ukajitahidi kuzama sana kwenye
mafuriko ya habari, basi, unaweza kukutana na habari nzito na za
kichambuzi haswa. Habari zitakazokufanya uelewe yale ambayo hukuyaelewa
kabla...
Yote hayo kwenye Nchi ya Wasadikika. Nchi yenye mambo ya ajabu.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam- Jiji kwenye Nchi ya Wasadikika
0754 678 252.inatoka http:www.mjengwablog.com
Comments