Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani.
Akizungumza leo mbele ya hadhara kubwa ya wananchi wa matabaka
mbalimbali kutoka mkoa wa Qum kwa mnasaba wa maadhimisho ya kutimia
miaka 36 tokea ilipojiri harakati kubwa ya kihistoria ya wananchi wa Qum
tarehe 9 Januari 1978, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameelezea
matamshi ya chuki yanayotolewa na shakhsia, duru za kisiasa na vyombo
vya habari vya Marekani yaliyo dhidi ya mfumo wa Kiislamu na wananchi
wa Iran, yakiwemo madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini na
kuongeza kuwa, kila mtu anazungumzia suala la haki za binadamu, lakini
Wamarekani hawana haki hata kidogo ya kuzungumzia suala hilo, kwani
serikali yao ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani.
Akielezea uungaji mkono unaofanywa na Marekani kwa utawala ghasibu wa
Israel katika jinai zinazotendwa na utawala huo dhidi ya wananchi wa
Palestina wakiwemo wakaazi wa eneo la Ukanda wa Gaza na hata kuwazuia
wananchi hao wasipate huduma za chakula na madawa, Ayatullah Khamenei
ameongeza kuwa, vitendo vyote hivyo vinaonyesha wazi ukiukaji wa haki za
binadamu unaofanywa na utawala huo ghasibu ukishirikiana na serikali ya
Washington.
Comments