Kifaru
cha kivita cha JWTZ kikifanya matayarisho ya mwisho kwa ajili ya
maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Gari
za Polisi zinazotumika wakati wa kuzuia vurugu katika maeneo mbali
mbali nchini zikipita mbele ya jukwaa kuu wakati zikiwa katika
maandalizi ya mwisho kwa ajili ya sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar zitakazofanyika Jan 12 katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Askari wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionyesha ukakamavu wao wakati wa
maandalizi ya mwisho ya maadhimisho ya kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Makomandoo
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { jwtz } wakionyesha ustadi wao wakati
wa mazoezi ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia nusu karne ya
mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Askari
wastaafu wa Jeshi la Ukombozi la Unguja (JLU) ambalo linatarajiwa
kuonyesha vitu vyao wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za
kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi
ya wanafunzi wa halaiki wa skuli mbali mbali za Zanzibar na Tanzania
Bara wakiwa katika mazoezi ya mwisho kujiandaa na sherehe za mapinduzi.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
----
Na Othman Khamis Ame
Jumapili
ya Januari 12 mwaka 2014 Watanzania wanatarajiwa kujumuika katika
maadhimisho ya kilele cha kutimia miaka 50 sawa na nusu karne ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Kilele
cha maadhimisho hayo kitafanyika katika tatan za uwanja wa Amani Mjini
Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi
Dr. Ali Mohammd Sheni atalihutubia Taifa uwanjani hapo hotuba itakayo
rushwa na kusikika moja kwa moja katika vyombo mbani mbali vya Habari
hapa Nchini.
Matayarisho
ya mwisho ya gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya majeshi yote
ya ulinzi Nchini Tanzania yamekamilika vyema katika uwanja wa amani
Mjini Zanzibar .
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na baadhi ya
wajumbe wa Kamati hiyo, maafisa wa vikosi vya ulinzi pamoja na baadhi ya
wananachi walishuhudia mazoezi hayo ya mwisho yanyiyoonekana kufana
sana.
Matayarisho
hayo yalikwenda sambamba na mazoezi ya ndege za Kivita za Jeshi la
Wananchi wa Tanzania { JWTZ } ambazo zilikuwa zikipita na kuonyesha
ustadi wake ndani ya eneo la mji wa Zanzibar kushajiisha umuhimu wa
maadhimisho hayo ya kihistoria.
Kazi
pevu na nzito iliyowaacha midomo wazi Makamanda, Viongozi na Mwenyekiti
mwenyewe wa Kamati ya Maadhimisho ya kitaifa Balozi Seif ilifanywa na
vijeba wa Jeshi la Wananchi wa Taznzania { JWTZ } wa Kikosi maalum cha
Makomandoo.
Ukafikia
wakati wa onyesho maalum la magari ya kivita ya jeshi la wananchi wa
Tanzania yaliyoongozwa na gari maalum zilizobeba baadhi ya silaha za
kivita kitendo kinachoonyesha umakini na umadhubuti wa Jeshi hilo.
Onyesho
hilo lilifuatiwa na lile la vikosi maalum vya askari polisi
vinavyohusika na mapambano dhidi ya wahalifu na wavunjaji amani ya Nchi
ambavyo baadhi ya wakati hulazimika kutumia mbwa , farasi na hata gari
za maji katika njia ya kurejesha hali ya amani hapa nchini.
Burdani
ya aina yake ikatokea ndani ya viwanja vya amani pale askari wastaafu
wa lililokuwa jeshi la ukombozi la Unguja { JLU } walipofanya vitu vyao
wakionyesha umahiri wao kwamba bado damu ya jeshi inaendelea kuwachemka
ndani ya miili yao.
Matayarisho
hayo ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yakahitimishwa
na watoto wa halaiki wapatao 2236 kutoka skuli mbali mbali za Zanzibar
na Tanzania Bara.
Watoto
hao waliweza kuufunika uwanja huo vitendo vilivyowafanya Viongozi na
makamanda walioshuhudia maajabu ya watoto hao yaliyoambatana pia na
sarakasi wasitulie katika viti vyao.
Comments