Jeshi la Nigeria limewatuhumu wanachama wa kundi la Boko Haram kuwa ndio
waliohusika na shambulio kubwa la jana Jumanne lililopelekea kuuliwa
makumi ya watu.
Ripoti zinasema kuwa watu wasiopungua 29 walipoteza maisha katika
mlipuko uliotokea sokoni hapo jana katika mji wa Maiduguri kaskazini
mashariki mwa Nigeria.
Muhammad Dole, msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa wanawashuku
wanachama wa Boko Haram kuwa ndio waliohusika na shambulio hilo la
mlipuko wa bomu.
Dole amesema makumi ya watu wameuawa na kujeruhiwa katika mlipuko huo wa
bomu uliotekelezwa na kundi la Boko Haram hapo jana katika mji wa
Maiduguri.
Comments