Arusha
Wanakwaya sita, waumini wa kanisa katoliki parokia ya Mt. Kalory Rwanga, Usa River, wamelazwa katika Hospitali ya Mission na Tengeru,wilayani Arumeru baada ya kujeruhiwa vibaya kwa bomu linalodaiwa kurushwa na askari polisi muda mfupi baada ya kutoka kanisani kwenye mkesha wa mwaka mpya.
PICHA KULIA :
Tukio hilo limetokea juzi majira saa 6.30 mita 100 kutoka katika kanisa hilo, eneo la Kisangani, ambapo waumini mbalimbali walikuwa wakielekea majumbani kwao baada ya kumalizika kwa misa ya mkesha.
Mganga msaidizi katika hospitali ya misheni,iliyopo chini ya kanisa hilo, Fredrick Mathew amethibitisha kupokea majeruhi watano, huku wawili wakiwa kwenye hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.
Aliwataja maheruhi hao waliolazwa hospitalia ya mission kuwa ni bi,Theresia Lesitare (33),bw Philipo Ambrose (22),bw Alphonce Nyigo (19)bi Mary Merikiory Kwai (40) na bi Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usariver.
Majeruhi mwingine ambaye hali yake sio nzuri, bi Annet Baltazar (16) amelazwa hospitali ya Tengeru.
PICHA KUSHOTO:
Alisema majeruhi hao waliumia sehemu za miguu na mapajani kwa kuchanwa chanwa na mlipuko wa bomu na baadhi ya vipande vya bomu vikitolewa kwenye miili yao na baadhi yao kushonwa kwa nyuzi kadhaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi wa tukio hilo umeanza mara moja na taarifa ya uchunguzi ataitoa baada ya kukamilika.

Askofu Josephat Lebulu wa jimbo kuu katoliki la Arusha
akiangalia kwa uchungu baadhi ya vipande vya bomu baada ya kutolewa kwa baadhi
ya majeruhi waliolazwa katika hospital ya Misheni, USA RIVER jana.
Tukio hilo limetokea juzi majira saa 6.30 mita 100 kutoka katika kanisa hilo, eneo la Kisangani, ambapo waumini mbalimbali walikuwa wakielekea majumbani kwao baada ya kumalizika kwa misa ya mkesha.
Mganga msaidizi katika hospitali ya misheni,iliyopo chini ya kanisa hilo, Fredrick Mathew amethibitisha kupokea majeruhi watano, huku wawili wakiwa kwenye hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.
Aliwataja maheruhi hao waliolazwa hospitalia ya mission kuwa ni bi,Theresia Lesitare (33),bw Philipo Ambrose (22),bw Alphonce Nyigo (19)bi Mary Merikiory Kwai (40) na bi Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usariver.
Majeruhi mwingine ambaye hali yake sio nzuri, bi Annet Baltazar (16) amelazwa hospitali ya Tengeru.
PICHA KUSHOTO:
Mwanakwaya ,bi Anna Methew akiwa
amelazwa katika hospital ya misheni baada ya kujeruhiwa miguuni na mapajani na
kushonwa nyuzi kadhaa.

Comments