Skip to main content

Kwenye nchi ya Wasadikika...



Mgeni unaweza kuwasikia wenyeji wakilalamika, kuwa mvua haijanyesha yapata miezi, na jua limekuwa kali mno, na joto pia. Lakini ajabu ya nchi ya Wasadikika, katikati ya jiji lao unaweza kukutana na madimbwi ya maji machafu, utadhani vile mvua kubwa imenyesha. Na hakuna anayejali.Wala magazeti ya nchi ya kusadikika hayaoni kuwa hiyo ni habari kubwa, maana inahatarisha afya za watu wa nchi ya Kusadikika. Magazeti ya Wasadikia yako bize na kuandika juu ya watu mashuhuri wakiwemo wanasiasa wa nchi ya Wasadikika.
Na ajabu nyingine ya Wasadikika watakaa wakijigamba kuwa wana Meya Wa Mji mahiri kama Meya wa New York City!
Maggid,
Mgeni kwenye Jiji la Wasadikika.Chanzo ni http://www.mjengwablog.com/

Comments