Polisi katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa Dar es Salaam, wanatajwa kuwa wahusika wakuu wa kusaidia
wahamiaji haramu kuingia nchini, kinyume cha sheria.Septemba mwaka jana,
mfanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali, Dominic Bomani alimwambia
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alipotembelea uwanjani hapo
kuwa wapo wahamiaji haramu ambao wamepewa nafasi nyeti za ajira katika
uwanja huo. Dk Mwakyembe aliahidi kufuatilia suala hilo.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa
polisi katika baadhi ya viwanja vya ndege wamejenga mtandao na watumishi
wengine, wakiwamo wa Idara ya Uhamiaji ambao huwawezesha raia wa kigeni
hasa kutoka nchi za Ethiopia, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC), kuingia nchini bila ya kuwa na nyaraka zinazokubalika
kisheria.
Tukio la karibuni zaidi ni lile la
kuingizwa nchini kwa raia watatu wa Pakistani ambao licha ya kukamatwa
katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal – I) kutokana na kutokuwa na
hati za kusafiria, wala nyaraka zozote zinazowaruhusu kuingia nchini,
baadaye waliachiwa na kuingia nchini katika mazingira ya kutatanisha.
Chanzo chetu uwanjani hapo kilisema:
"Hawakuja na hati za kusafiria wala nyaraka zozote na waliachiwa huru
katika mazingira ya kutatanisha."
Chanzo hicho kiliwataja Wapakistani
hao kuwa ni Hussein Amir, Ahmad Tahmir na Shakeel Muhamadadi ambao
walifika nchini, Oktoba Mosi, 2013 saa kumi na moja jioni kwa ndege
ndogo ya kukodi ambayo ilikuwa ikitokea Zanzibar.
Baada ya kufika, walishukia Terminal 1
na baadaye kwenda kuswali katika msikiti wa karibu, lakini kabla ya
kutimiza azma yao hiyo, walikamatwa na polisi kisha kufunguliwa hati ya
kukamatwa (RB) namba JNIA/1005/2013.Soma zaidi...
Comments