NA FRANCIS GODWIN:
MAELFU ya
wakazi wa mkoa wa Iringa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na
Serikali wakiongozwa na Rais Dr Jakaya Kikwete wameshiriki katika
mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga na waziri wa fedha Dr
Wiliam Mgimwa.
Huku
waziri mkuu Mizengo pinda katika salam zake za serikali akielezea jinsi
ambavyo Taifa lilivyopata pigo kubwa kufuatia kifo cha Dr Mgimwa
kutokana na mchango wake katika baraza la mawaziri.
Katika
mazishi hayo yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga jimbo la Kalenga
wananchi mbali mbali walionyesha kujipanga barabarani kutoka Manispaa ya
Iringa hadi kijijini kwake huku wakiupungia mkono msafara wa rais
Kikwete na baadhi yao wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na
pikipiki kwenda katika mazishi hayo.
Akitoa
shukrani za familia kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu Dr Mgimwa
Godfrey Mgimwa aliishukuru serikali kwa jinsi ambavyo ilivyohangaika
kumuuguza baba yake na kutoa wosia mzito wa marehemu Dr Mgimwa ambao
alimtaka kuufikisha kwa Rais Kikwete..
Alisema
katika uhai wake kabla ya kifo chake ikiwa ni siku tano kabla Dr Mgimwa
alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais Kikwete kwa
kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa pamoja na spika wa
bunge Anne makinda .
Pia
alisema kuwa alieleza dhamira yake ya kuwatumikia wana Kalenga na kusema
zawadi kubwa ni msaada wa bati zaidi ya 2000 kwa wananchi hao ili
kuendeleza ujenzi wa shule na vituo vya afya jimboni.
"Baba
kabla ya kufa aliniachia wosia huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru
kwa ushirikiano wao na kutoa bati ila alipenda kuona Kalenga inakuwa na
maendeleo zaidi"
Kwa
upande wake waziri Mkuu Pinda alisema kuwa serikali imepata pigo kubwa
juu ya kifo hicho na kuwa bado serikali itaendelea kuwa karibu na
familia ya Dr Mgimwa na pale penye tatizo isisite kuwasiliana .
Hata
hivyo Rais Kikwete hakupata kuzungumza chochote katika msiba huo zaidi
ya kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono ndugu wa Dr
Mgimwa .
Spika wa
bunge Anne Makinda alisema kuwa bunge limempoteza kiongozi na mbunge
aliyependa kutumia nafasi yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe mchango
wake hawataacha kuukumbuka.
Comments