(via wavuti website) HALI ya taharuki jana iliwakumba wakazi wa eneo la Shekilango, jijini Dar es Salaam, baada ya kuona kitu aina ya chuma kilichokuwa kimejifukia ardhini na kuonekana sehemu ya juu, wakidhani kuwa ni bomu. Taharuki hiyo ilizuka majira ya saa 3:00 asubuhi.
Hata hivyo, Polisi baada ya kupata taarifa, walifika katika eneo hilo na kukifukua kitu hicho na kuondoka nacho kwa ajili ya kukifanyia uchunguzi.
Comments