Muhubiri
wa kanisa la Seventh Day Adventist nchini Rwanda, Nicolas Niyibikora
huenda akajikuta mikononi mwa polisi mara baada ya kudai kuwa wanawake
ndio chanzo cha maovu ulimwenguni.
Kupitia mahubiri Yake
yaliyorushwa na kituo cha redio cha Amazing Grace, Niyibikora aliwambia
wanawake kwamba hawapendwi na Mungu na kuonya kuwa hakuna lolote jema
linaloweza kupatikana kutoka kwao.
Kutokana na mahubiri hayo
kukasirisha wengi kanisa la Seventh Day limefanya juhudi za kujitenga
na Niyibikora ambaye wanadai aliipigwa marufuku kwa miaka mitano
iliyopita.
Kwa mujibu wa gazeti la New Times tayari mahubiri hayo
yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa
kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo
kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa
Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa.
Comments