Serikali itakayo punguza au kumaliza changamoto zinazowakabili wanawake wanaofanya biashara mipakani mwa nchi
SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano nchini imeshauriwa kutunga sheria itakayo punguza au
kumaliza changamoto zinazowakabili wanawake wanaofanya biashara mipakani mwa
nchi.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam juzi na wadau wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP
) ambapo ushauri huo umetolewa na washiriki wa mafunzo ya kuzingatia masuala
ya kijinsia katika biashara za mipakani yaliyoendeshwa
na mtandao huo.
Baadhi ya changamoto zizoelezwa wakati wa mafunzo hayo ni
zile zinazolenga kumdharirisha mwanamke awapo katika harakati za kuendesha
biashara zake katika maeneo ya mipakani.
Moja ya changamoto zilizoelezwa moja wapo ni kuombwa rushwa ya ngono ,upekuzi
wa maungoni usio zingatia jinsi,mwanamke kupekuliwa na mwanaume na hivyo
kushauri serikali iajiri ma askali wanawake katika mipaka hiyo kwa uwiano sawia
kati ya mwanamke na mwanaume ili kisiwepo kisingizio,
Pia ni urasimu umeelezwa
kuwa ni changamoto nyingine kwa watumishi wa serikali waliopo mipakani
kwa pande zote mbili yaani nchi na nchi hususani maaskari wanatuhumiwa kuwa na
urasimu katika utoaji wa huduma na kutafuta visingizio na hatimaye mwanamke
kujikuta ametoa rushwa ya ngono.
Hata hivyo imebainika kuwa wanawake wengi hawajiamini na
hawafuati ama kusoma miongozo ya biashara sanjari na hilo wanawake hufanyiwa
ukatili wa kijinsia wawapo mipakani.
Hivyo kupendekezwa kuwa watoa huduma mipakani wajengewe uwezo
kuhusu biashara mipakani hivyo wizara washirika watoe elimu kulingana na kada
zao mana biashara ni suala mtambuka ambapo hugusa sekta nyingi.
Kwa upande wake Ofisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na
Biashara Fredy Kakula alisema kuwa kuna kila sababu Serikali kutunga sheria
itakayotoa Muongozo wakuendesha biashara mipakani kwa wanawake.
“Kwasasa tunaongozwa na sera,na sera yenyewe ilitungwa mwaka
2003 ni takribani miaka 15 sasa hatuna budi kutunga sheria na sera mpya dhidi
ya wanawake wanaofanya biashara mipakani.Kakula alisema.
Naye Mhamasihaji toka TGNP Gemma Akilimali amewataka
washiriki hao kwenda kupigia chapuo katika Wizara wanazo hudumu ili iweze
kufanyiwa kazi haraka mana athari zitokanazo na ukatili wa mwanamke mfanya
biashara mpakani zinaongezeka kila siku.
‘’Pamoja na TGNP kuchagiza katika hili bado mchango wenu ni
mkubwa katika kufanikisha hili kwakuwa nyiynyi ndiyo mpo jikoni.
TGNP imekuwa ikitoa semina mbali mbali za kuwajengea uwezo
makundi ya jinsia na kwa lika tofauti bila kujali kijana au ,mzee ama mwanamke
au mwanaume.
Comments