TIMU
ya El Masry imeanza vyema Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi
wa 4-0 dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia kwenye mchezo wa kwanza wa
Raundi ya Kwanza juzi mjini Cairo.
Masry,
inayofundishwa na gwiji wa Misri, Hossam Hassan juzi ilicheza katika
Uwanja wake wa nyumbani, Port Said kwa mara ya kwanza baada ya miaka
mitano ya kucheza ugenini kufuatia kufungiwa kwa sababu ya vurugu mwaka
2012.
Ikumbukwe,
Masry wakivuka raundi hii watakutana na mshindi wa jumla kati ya Simba
ya Tanzania na Gendarmerie Tnare ya Djibouti. Simba nayo jana ilishinda
4-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
Mabao
ya Masry yalifungwa na Islam Salah dakika ya 14, nyota wawili kutoka
Burkina Faso Aristide Bance dakika ya 40 na Mohamed Koffi dakika ya 52
na Islam Issa dakika tisa kabla ya filimbi ya mwisho.
Masry sasa watasafiri kuwafuata Green Buffaloes kwenda kuulinda ushindi wao huo kwenye mchezo wa marudiano Februari 20.
Comments