Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam(picha na blog hii)
Watanzania pamoja na wadau mbalimbali nchini wamekumbushwa kulinda,kuhifadhi na kuendeleza historia ya ukombozi wa bara la Africa ili kukuza na kuleta tija hapa nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati akifanya ziara ya kutelembelea Jengo la Makumbusho ya Ukombozi wa Bara la Africa jijini Dar es salaam.
Dkt Mwakyembe amesema Tanzania imepewa jukumu zito na Umoja wa Afrika kuhakikisha wanasimamia na kuhifadhi historia ambazo zimesababisha ukombozi wa bara la Afrika.
Kwa Upande wake Msimamizi Mkuu wa mradi wa Urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika bi,Ingiahed Mduma amesema wanatarajia kutengenezaneza mradi mkubwa wenye lengo la kuitangaza Tanzania kupitia utalii.
Jengo hilo ambalo ndio makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ya OAU ilianza mwaka 1969 baada ya kamati hiyo kukamilisha jukumu lake la ukombozi wa bara ziuma la Afrika na hivyo mnamo Novemba 4,1994 lilikabidhiwa kwa JWTZ ili litumike kama makumbusho ya Historia ya Jeshi pamoja na makumbusho ya Ukombozi.
Comments