Mbunge wa Chalinze kupitia tiketi ya CCM, Ridhiwan Kikwete ni moja ya
viongozi waliohudhuria kwenye kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa
jimbo la Kinondoni kumnadi Mgombea wa chama hicho, Maulid Mtulia na
kuwaasa wananchi wa jimbo hilo kumchagua Maulid Mtulia.
Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kinondoni wanapaswa kumchagua Mtulia
kama kiongozi wao kwani yeye atakuwa daraja kati ya wananchi na
Maendeleo.
“Kinondoni tunachagua (Maulid Mtulia) Daraja litakayeunganisha wananchi na Maendeleo, #hapakazitu,”ameandika Mhe. Ridhiwan Kikwete kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Marudio ya Uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Februari 17, 2018.
Comments