CHUO Kikuu Huria kimesaini Makubaliano yanayo husisha Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Kimataifa ya Ushirika wa Vijana(IYF)
Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Kimataifa ya Ushirika wa Vijana(IYF)
Akizungumza wakati wa makubaliano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Chuo Kikuu hicho Jijini Dar es Salaam ambapo
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Elfas Bisanda amewataka Vijana
nchini kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi, kuliko kukaa vijiweni
wakipga soga nakujingiza katika ulevi wa madawa ya kulevya.
Alisema Makubaliano hayo yamehusisha IYF na Chuo hicho ambapo
Asasi hiyo itakuwa ikiwafundisha walimu wa chuo hicho elimu ya moyo
wakujitambua ijulikanayo kama badilisha mtazamo.
Lengo la elimu hiyo ambayo itaingizwa katika mitaala ya Chuo hicho
nikubadilisha mtazamo wa vijana kuhusu mambo mbali mbali yanayo
wahusu vijana hususani ajira.
Prof Bisanda amesema kuwa katika ufanyaji kazi wa pamoja watashirikiana
zaidi katika malezi ya mtazamo wa vijana katika masuala ya kimataifa
nakuongeza kuwa somo hilo la moyo wa wazi litawajengea uwezo na uwelewa
wakutosha wanafunzi.
“Kimsingi wanafunzi ,walimu na jamii itanufaika na elimu ya Badilisha
fikra itakayotolewa na ndugu zetu kutoka Korea ya Kusini hivyo watanufaika
lakini wanafunzi zaidi watapanua wigo wa ajira kimataifa kuliko ilivyo sasa.
Hata hivyo amewaasa Vijana wakitanzania kujituma zaidi nakufanya kazi za
kujitolea ambazo badaye zitawafanya waajiriwe kutokana na soko la ajira
kuwa gumu ulimwenguni kwa nyakati hizi.
“Vijana wengi hawataki kujitolea au kufanya kazi kwakujituma wanapenda
kujiingiza katika makundi ya siyofaa ,rai yangu vijana wafanye kazi
kwakujitoa zaidi na mengineyo yatafuata.Alisema Prof Bisanada.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa IYF kutoka Makao Makuu ya Asasi hiyo yaliyopo
Korea ya Kusini Profesa Kim Seong Hun amesema kuwa kuingizwa kwa mtaala
wa badilisha fikra utakaofundishwa Chuoni hapo utakuwa na mchango mkubwa
sana kwa jamii kubwa nchini Tanzania.
“Nje ya kufundisha walimu na wanafunzi tunakuwa na makambi kila mwaka hapa
nchini kwa wanafunzi na walimu wa sekondari na vyuo vikuu hivyo kuwajengea
uwelewa wakukabiliana na changamoto mbali mbali.Alisema Prof Kim.
Prof Kim ameongeza kuwa,vijana watanzania wakutanishwa na vijana wengine
kutoka nchi 86 Duniani huko Korea ya Kusini katika mkutano mkubwa ambao
hujadili changamoto zao bila kulipia chochote ambao hufanyika kila mwezi
wa saba katika mwaka.Alisema Prof Kim.
Sanjari na hafla hiyo fupi ya utiaji saini hati ya makubaliano ambapo IYF
watatoa utaalamu wa ufundishaji na vifaa vyakufundishia ,wakati huo huo
walimu wakuu wa sekondari na msingi zaidi ya 600 kutoka shule mbali mbali
za Dar es Salaam walijengewa uwezo wa Badilisha fikra chuoni hapo.
Comments