Wachezaji na benchi la ufundi la Singida United wakishagilia goli la Deusi Kaseke
Mabingwa
wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC wameiengua Yanga SC kwenye nafasi
ya pili waliyoishikilia kwa muda kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya
Lipuli.
Azam wamerejea kwenye nafasi hiyo baada
ya kuwachakaza Ndanda FC kwa kipigo cha mabao 3-1 kwenye mchezo
uliopigwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
Yahya Zayd, Enock Atta na Shaban Chilunda huku bao la kufutia machozi likifungwa na Nasoro Kapama.
Wakati hayo yakitokea Dar es Salaam,
huko Iringa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC
wameweka historia mpya kwenye uwanja wa Samora baada ya kupata ushindi
wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya wenyeji wao Lipuli.
Yanga ilipata mabao yake kwenye kila
kipindi huku kiungo Papy Kabamba Tshishimbi akiwa wa kwanza kuiandikia
bao mnamo dakika ya 18 kwa kumalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa
Lipuli kufuatia jaribio la Emmanuel Martin.
Kipindi cha pili, Pius Buswita
aliihakikishia Yanga ushindi kwa bao maridadi akimalizia krosi ya chini
chini iliyopigwa na Obrey Chirwa kabla ya kumpiga chenga kipa wa Kipuli
na kuukwamisha mpira kimiani.
Michezo mingine ya VPL itaendelea kesho
ikiwemo mchezo wa Mtibwa Sugar itakayoukuwa mgeni wa Stand United ‘Chama
la wana’ kwenye mechi inayotarajiwa kuanza saa 8.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Singida United 3 – 2 Mwadui
Majimaji 1 – 2 Mbeya City
Tanzania Prisons 2 – 0 Njombe Mji
Comments