WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amefunga mabao matatu, timu yake, Difaa Hassan El Jadida iksihinda 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.
Msuva aliye katikaa msimu wake wa kwanza klabu hiyo baada ya kujiunga nayo kutoka kwa mabingwa wa Tanzania, Yanga SC alifunga mabao yake katika dakika za 44, 72 na 88.
Sasa akina Msuva watakwenda ugenini Guinea Buissau katika mchezo mwepesi kabisa baada ya ushinsi huo mnono wa nyumbani.
Comments