Wakati alipoifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili, mshabuliaji Jesse Lingard alishangilia katika namna ambayo mikono yake iliunda ishara ya herufi JL.
Herufi J ilikuwa ikiwakilisha jina la kipenzi chake Jena Frumes wakati L iliwakilisha Lingard.
Lingard alishangilia kwa staili hiyo ya kipekee kabla ya kwenda kuungana na swahiba wake Paul Pogba na kutengeneza ishara ya 'Wakanda Foreva' kutoka katika filamu inayoingisha dunia kwa hivi sasa "Black Panther".
Katika kujibu mapigo ya mpenzi wake, kimwana Jena Frumes naye akaingia dukani na kutengeneza kidani kilichokuwa na ishara ile ile ya ushangiliaji wa Lingard.
Comments