Imeelezwa , Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe kujitetea.
Akiongozwa na Mawakili Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza kutoa utetezi wake leo Masogange ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.
Masogange anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.
Akijitetea Masogange alidai kuwa mbali ya ‘Uvideo Queen’ pia alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.
Alidai kuwa Februari 14,2017 polisi walienda
nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa
amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.
Masogange katika kesi hiyo anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14,
2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam
alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia, anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Comments