Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kugharamia mazishi ya mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji (NIT), Akwilina Akwelina
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kugharamia mazishi ya mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji (NIT), Akwilina Akwelina aliyeuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa Februari 16, 2018 wakati wa maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishinikiza Mkurugenzi wa Uchaguzi Kinondoni kutoa viapo kwa mawakala wa chama hicho.
Hayo yamesemwa leo Jumapili Februari 18, 2018 na Waziri wa Elimu na
mafunzo ya ufundi, Prof Joyce Ndalichako alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
“Serikali imepata pigo kwani inawekeza fedha nyingi kusomesha
wanafunzi na marehemu Akwilina alikuwa ni miongoni mwa wanufaika wa
mikopo ya elimu ya juu, tutagharamia shughuli zote za mazishi ya
marehemu hadi atakapopumzishwa katika makao yake ya milele,“amesema Prof. Ndalichako huku akitoa onyo kwa Watanzania kuhusu maandamano.
“Nawasihi watanzania kujiepusha na maandamano na vitendo vyote ambavyo vinaweza kusababisha uvujifu wa amani,“Prof. Ndalichako.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments