WINGA
wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amefunga
mabao matatu, timu yake, Difaa Hassan El Jadida iksihinda 10-0 dhidi ya
Benfica ya Guinea Bissau katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza
Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida,
Mazghan nchini Morocco.
Msuva
aliye katikaa msimu wake wa kwanza klabu hiyo baada ya kujiunga nayo
kutoka kwa mabingwa wa Tanzania, Yanga SC alifunga mabao yake katika
dakika za 44, 72 na 88.
Mabao
mengine ya Difaa Hassan El Jadida yalifungwa na Bakary N'diaye dakika
ya nne, Hamid Ahadad dakika za 23, 26, 37, 42 na 47 na Bilal El Magri
dakika ya 54.
Sasa akina Msuva watakwenda ugenini Guinea Buissau katika mchezo mwepesi kabisa baada ya ushinsi huo mnono wa nyumbani.
Comments