Beki wa klabu ya Simba, Salim Mbode, jana amerejea rasmi mazoezini ndani ya kikosi hicho baada ya kupona majeraha ya goti.
Mbonde alikosekana katika kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar FC, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba, zinzeleza kuwa Mbode ameanza mazoezi leo akiwa chini ya Mwalimu wa Viungo, Mohammed Hbibi, pamoja na Daktari wa timu, Yassin Gembe.
Mbonde amerejea mazoezini ikiwa Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC, ukaochezwa kesho Jumatatu jijini Dar es Salaam.
Comments