Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amempa 'tano' kocha wake Jurgen Klop kwa mafanikio anayoyazoa msimu huu.
Salah
amefunga magoli 30 katika mechi 36 za michuano yote katika msimu wake
wa kwanza na Liverpool na ni mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwa
upachikaji mabao Premier League akiwa na magoli 22, nyuma ya Harry Kane
mwenye magoli 23.
"Liverpool
nimekuwa nikicheza jirani zaidi na lango la adui, kocha wangu amenitaka
nicheze hivyo, hatua inayoniwezesha kupachika magoli mengi," anaeleza
Salah na kuongeza: "Sikuwahi kupewa fursa hiyo katika klabu nyingine yoyote ile au kwa kocha mwingine kabla ya kukutana na Jurgen Klop"
Comments