Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi.
Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa.
Rais Muhammadu Buhari ameelezea tukio hilo kama janga la taifa.
Hasira zimekuwa zikiwapanda wazazi wa wasichana hao huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa kutoka kwa vizuizi vikuu vya Dapchi mwezi uliopita.
Dampchi ambao ni mji ulio kilomita 275 kaskazini magharibi wa Chibok, ulishambuliwa siku ya Jumatatu, na kusababisha wanafunzi na walimu kutoka shule moja ya serikali kukimbiliaa vichakani.
Wenyeji wanasema vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiw na ndege za vita baadaye vilizima uvamizi huo.
Mamlaka awali zilikana kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa, zikisema kuwa walikuw wamejificha kutoka kwa wanamgambo hao.
Lakini baadaye wakakiri kuwa wasichana 110 walikuwa hawajulikani waliko baada ya uvamizi huo.
Comments