Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya Luteni Jenerali Yakubu Hassan
Mohamed ambapo awali alikuwa na cheo cha Meja Jenerali kabla
hajamuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed
kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Luteni
Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akila Kiapo cha kuwa Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali
Yakubu Hassan Mohamed akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati Maafisa Mbalimbali wastaafu
wa (JWTZ) walipokuwa wakizungumza mara baada ya tukio la uapisho Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed mara
baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi mbalimbali
wa habari waliofika kuripoti habari za Uapisho wa Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu
Hassan Mohamed Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa
Mbalimbali wa Jeshi waliopandishwa vyeo kutoka Brigedia Jenerali na
kuwa Meja Jenerali wakipiga makofi wakati wa hotuba za Maafisa
mbalimbali wastaafu wa JWTZ walipokuwa wakizungumza Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo
akiwavalisha vyeo vipya vya Meja Jenerali kutoka Cheo cha Brigedia
Jenerali maafisa mbalimbali wa Jeshi hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali
Yakubu Hassan Mohamed mara baada ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa
Mbalimbali wa Jeshi la Wananchi akiwemo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan
Mohamed watano kutoka kulia wakiwa wamepiga Saluti wakati Wimbo wa Taifa
ukipigwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi
Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania
(CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed pamoja
na Maafisa wengine wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi ambao wamepandhishwa
vyeo kutoka Cheo cha Brigedia Jenerali na kupewa cheo kipya cha Meja
Jenerali Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments