BEKI wa Simba, Shomari Kapombe ameuzungumzia mchezo wao na Mwadui FC, kwamba utakuwa mgumu ila wanahitaji kupambana ili kuwaacha mbali wapinzani wao wanaofuatana kipointi.
Kapombe anasema Mwadui ni timu ngumu, inayotakiwa wacheze kwa uangalifu ili waweze kushinda mchezo huo utakaofanya wazidi kuwa mbali zaidi kipointi.
"Kila mechi tunaichukulia kama fainali,tunafanya hivyo ili tuweze kufikia ubingwa ambao kila shabiki ana hamu kuona linatia hilo,"anasema.
Anasema ugumu wa mechi huo unatokana na baadhi ya timu zinataka zisishuke daraja, nyingine zimalize nafasi za juu na zile ambazo zinawania ubingwa.
Comments