Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba, hii leo itaingia uwanjani kutupa karata yake dhidi ya Mbao FC mchezo utakao pigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kuelekea kwenye mchezo huo uliyokuwa muhimu zaidi kwa upande wa Simba SC katika kujihakikishia inajikusanyia pointi nyingi zaidi ili kuwa mbali na hasimu wake wa jadi Yanga SC, tayari wametaja kikosi kitakacho shuka dimbani leo hii.
Simba SC wanaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 42 dhidi ya 37 ya Yanga SC inayoshika nafasi ya pili.
Comments