Mawakili nchini Kenya kupitia chama cha wanasheria nchini LSK wameahairisha mgomo wao ili kutenga muda Zaidi kwa maandalizi ya mgomo huo. Mgomo huo ulioelezwa kuwa ni kulalamikia mazoea ya serikali kuu nchini humo kukaidi agizo la mahakama na vile vile kuidharau idara ya Mahakama ulipangwa kufanyika jumatatu hii ya Februari 12 na ungedumu kwa muda wa siku tato.
Chama hicho cha wanasheria nchini LSK kimetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kusitisha mgomo wao kwa muda ili kutenga nafasi zaidi ya mashauriano kuhusu maandano.Pia, walishtumu serikali kuu kukiuka haki za waliotiwa mbaloni na kutumia idara ya polisi visivyo kukandamiza wananchi wa Kenya bila sababu dhabiti.
Kupitia kwa taarifa ya LSK kwa vyombo vya habari, wamehoji kwamba, wamechukua hatua ya kisitisha mgomo huo kwa muda ili kutenga nafasi ya mashauriano zaidi.
Mgomo huo ulitarajiwa kuathiri mahakama zote isipokuwa zile zinazoshugulikia kesi za uchaguzi, ambapo mawakili wangevaa mikanda ya njano wakati wa mgomo huo.
Hatua hii ya mawakili yamejiri siku chache baada ya serikali kuu kupitia kwa mamlaka ya mawasiliano nchini kuzima mitambo ya runinga za Citizen, KTN, NTV na Inooro kufutia hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinda. Mahakama baadaye iliamuru mitambo hiyo ifunguliwe lakini serikali ikakaidi agizo hilo.
Comments