Teknolojia mpya ya huduma ya Usafiri kwa njia ya mdandao (UBER)
ilizindua, uzinduzi wa Stika za magari kwa madereva wanao tumia
kusafirisha abiria .
Kutokana na harakati hizo za kutumia usafiri huo, jiji
la Dar es Salaam limetajwa kuwa limetangulia kuwa mstali
wa mbele kwa haraka kutokana na ubunifu huo wa mfumo
wa kisasa.
Hayo yalisemwa jijini hapa juzi na meneja wa UBER nchini
Alfred Msemo katika mazungumzo na waandishi wa habari yaliyofanyika
katika hotel ya Serena .
Alfred alisema Dar es Salaam ni kivutio kikubwa cha utalii,
nakuwa wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Mstahiki Meya
wa jiji.
"Sasa halmashauri ya jiji hili itawataka madereva wanaotumia
programu ya UBER kulipa Shilingi elfu 80,000 kabla ya kupewa
Stika ambapo Stika hiyo itadumu kwa muda wa mwaka mmoja,"alisema
Alfred.
Alfred Meneja huyo alisema hiyo ni hatua muhimu na ni ushahidi wa
juhudi zinazofanywa na UBER katika kushirikiana na halmashauri
za miji mbali mbali katika mchakato wa kuunda sera zinazo walenga
madereva wa UBER.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
aliipongeza kampuni ya UBER aliipongeza kampini hiyo wakati
wa uzinduzi huo.
"Zaidi ya watu 1ooo wamepata ajira mpya ya kutengeneza pesa
huku watu zaidi ya elfu kumi (10), wakitumia usafiri huo kwenye
mizunguko yao,"alisema Isaya.
Alisema kwa sasa watu wameshuhudia teknolojia hiyo ya UBER
kwani tayari imeleta mafanikio makubwa hususani kwenye
suala zima la usalama.kuvutia watalii, pamoja na kupunguza
foleni za msongamano bara barani.
Vile vile Meya Isaya alisema jiji la Dar es Salaam ni mji unao
fikiria kwenda mbele zaidi na kwenda na wakati na ndio maana
wameonesha kuwa wapo tayari kuwa na aina mpya ya biashara kama
UBER nakuwa Madereva wote wanaoitajika kutoa huduma hiyo,wataitajika
kuwa na stika kutoka jiji la Dar es Salaam.
Naye Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini
SACP.Fortunatus Musilimu alisema Jeshi la Polisi litashirikiana
na Kampuni ya UBER nchini kupitia madereva wao kupata taarifa
za uhalifu na wahalifu na kuzifanyia Uchunguzi kwani madereva hao
muda mwingi wapo barabarani.
SACP.Fortunatus alisema kuwa UBER kuwa ni kama wadau wengine weledi
katika kuzuia ajali za barabarani,uhalifu na waalifu.
"Kupitia Stika hizo, zinazozinduliwaleo (juzi) tutaweza kujua magari
yanayofanya biashara kwa kutumia teknolojia na kutumia teknolojia
hiyo katika upelelezi wa matukio ya ajali na uhalifu,"alisema SACP.
Fortunatus.
Tayari Kamanda huyo wa Polisi ametaja kuwa kufikia mwaka 2017 UBER
imetoa jumla ya ajira 6,000 za madereva ambapo jumla ya wateja 28,000
wamepata huduma nzuri kwa njia ya mtandao (APPS) na jumla ya wateja kutoka
mataifa mbali mbali .
Comments