Taasisi isiyokuwa ya
Kiserikali ya Kimataifa ya Ushirika wa Vijana(IYF) ,imezindua mpango wa ajira
kwa vijana nje ya nchi.Uzinduzi huo wenye kauli mbiu Najivunia Tanzania
umezinduliwa jana Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa wakati wa
uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dare es
Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa IYF Chung Yang alisema lengo la mpango huo nikuunga
mkono Serikali katika jitihada za kupambana na tatizo la ajira
“Hakuna asiyejua kuwa
kuwa kuna shida ya ajira ,Serikali ilikuwa ikiomba sekta binafsi kuibua ajira
kwa kwa vijana na sisi tumeamua kuja na
mpango huu wa ajira ya kujitolea nje ya nchi ambapo watapata uzoefu katika anga
za kimataifa na uzoefu .Alisema Yang.
Yang amesema
wameichagua Tanzania kutokana na ukweli usiopingika kuwa vijana wengi
wakitanzania ni waadirifu na wapo tayali kujitoa hivyo wameona ni vema kuwekeza
nguvu zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine.
Pichani ni Mkuu wa IYF Chung Yang akielezea wadau waliojitokeza katika ukumbi huo Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dare es Salaam leo.
Vijana hao
wanaotarajiwa kwenda kufanya kazi katika nchi mbali mbali idadi yao itajulikana
hivi karibuni kulingana na uhitaji wa chi husika.Vijana hao watapatiwa hati ya
kusafiria,Visa,na watalipiwa usafiri nakugharamiwa mahitaji yote ya msingi kama
chakula malazi, na mahitaji mengine na pesa za kujikimu wawapo nchi za nje.
Kulia ni Yang akiwa na Seong Hun Kim katika mazungumzo na wanahabari Nkuruma Hall.
Kwa mujibu wa Yang
nchi kati ya 25 hadi 30 zimeonesha utayali wakuchukuwa Vijana wakitanznia
kufanya kazi katika nchi mbalimbali kati ya nchi 86 ambapo IYF ina hudumu.
Kipepe rushi kilichokuwa kiki muonesha kijana wa kitanzania Velence Mkulu.
Kijana Velence Mkulu akizungumza na wanahabari leo
Kwa upande wake
Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Paulina Mabuga ,alisema kuwa
mpango huo ni mzuri na kwa chuo Kikuu Cha Dar es Salaam umekuja wakati muafaka
,wakati ambao wahitimu wengi hawana ajira.
“Kwetu sisi ni faraja
kubwa ,madhumuni ya chuo ni kuandaa wahitimu wanaolitumikia Taifa na Dunia
haipendezi kuona vijana wengi hawana ajira,Hata hivyo UDSM tuna mpango kama huo
ambapo tunawabakisha wanafunzi kwa ajiri ya kuwaelekeza wenzao hususani mwaka
wakwanza na badaye huajiriwa.Alisema Paulina.
Mwazani Ramadhani ni
miongoni mwa wanufaika wa mpango wakujitolea nje ya nchi ambapo alifanya kazi
Kenya kwa miezi 3 na Korea ya
Kusini miezi 6 anaeleza ni jinsi gani
mpango huo umewasaidia.
“Kutokana na soko la
ajira kuwa tete mpango huu ni mkombozi kwanza umenipatia uzoefu wa kimataifa
lakini umeniongezea wigo mkubwa na ufanisi katika kazi mbali mbali ikizingatiwa
wenzetu wapo mbali kimaendeleo hata kitekinolojia.
Mwazani ameongeza kuwa
watu wanakuwa na mitazamo hasi kuhusu watu weupe(watu wa ughaibuni)hususani
kaitika suala la ubaguzi wa rangi kwa Korea ya Kusini haikuwa hivyo wanawapenda
sana waafrika.
Kwa upande wake
Valence Maluku mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia Cha Dar es Salaam ni miongoni
mwa wanufaika aliyefanya kazi Uruguai kwa mwaka mmoja anasema pamoja na kwamba
nchi za Amerika ya Kusini zina ubaguzi mkubwa wa rangi lakini yeye ameshinda
vita kutokana na Taasi ya IYF kuwalea vizuri hivyo hakupata shida yoyote.
“Nilikuwa nikitoa
elimu kuhusu athari zitokanazo na madawa ya kulevya kwa kiasi Fulani nilifaidika
ikiwemo kujifunza kispaniola na kiruguai lakini nmesafiri nchi kadhaa kama
Marekani,Agentina na Brazili katika mikutano mbali mbali.Alisema Maluku
Wanufaika hao wote kwa
pamoja wanazungumzia changamoto ya lugha kuwa shariti ujifunze lugha na
huwalazimu kujifunza kati ya miezi mitatu hadi sita ndipo unapoelewa kwa
ufasaha.
Kuhusu suala la
usalama wao wamekiri kuwa hawakuwa na shida ya tatatizo la usalama kwakuwa
walikuwa chini ya usimamizi mzuri na Salama.
Sifa zinazohitajika ni
kijana yeyote wakitanzania kuanzia miaka 18 hadi 35 ,ambapo hupatiwa mafunzo
katika makambi mbali mbali nchini ,chini ya IYF na huwa na hiari yakuchagua
nchi waipendayo.
IYF hufanya kazi kwa
ukaribu na ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya Mambo ya ndani,Wizara Ushirikiano wa
Kimataifa Kikanda na Wizara ya Tamisemi.
Comments