Liverpool
imeshindwa kulinda mara mbili uongozi wake katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
dhidi ya Tottenhm na kuambulia sare ya 2-2.
Kikosi cha Jurgen
Klopp kilipata bao la mapema kunako dakika ya tatu mfungaji akiwa ni Mohamed
Salah.
Kwa muda wote wa
kipindi cha kwanza Liverpool walicheza soka la kuonana na kama washambuliaji
wake wangekuwa makini wangeweza kupata bao lingine.
Kipindi cha pili,
kibao kikageuka ambapo Tottenham wakaweka kambi kwenye nusu ya Liverpool ambayo
iliamua kupaki ‘treni’ ili kulinda bao lao kwenye uwanja wao wa nyumbani - Anfield.
Licha ya
Liverpool kufanikiwa kulinda lango la kwa muda mrefu, lakini dakika ya 80
kiungo Victor Wanyama akafanikiwa kuizawazishia Tottenham kwa shuti kali la nje
ya box la 18 baada ya piga nikupige.
Liverpool ikiwa
inaendelea kucheza soka la kujihami ikajikuta inaruhusu penalti dakika ya 87
ambayo ilipigwa na Harry Kane lakini ikaokolewa na kipa Loris Karius.
Dakika ya kwanza
katika nne za majeruhi, Liverpool wakafanikiwa kufunga bao la pili lililofungwa
na Mohamed Salah baada ya shambulizi la kushitukiza.
Wakati Liverpool
wakiamini wameshinda mchezo huo, Tottenham ambayo ilimiliki mpira kwa asilimia
66, ikasawazisha sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho kupitia penalti
iliyopigwa tena na Harry Kane.
Comments