MPULIZAJI tarumbeta nguli, Hamis Mnyupe amerejea kwenye bendi yake ya zamani ya Msondo Ngoma Music Band na tayari ameanza kuonekana kwenye shoo za bendi hiyo tangu wiki iliyopita.
Mnyupe aliyewahi kuitumikia Msondo Ngoma kwa zaidi ya miaka kumi na tano, aliipa kisogo bendi hiyo takriban miaka miwili iliyopita, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni maslahi na kubadilisha upepo.
Kiongozi mwandamizi wa Msondo Ngoma, Juma Katundu ameiambia Saluti5 baada ya kuona kwamba bendi yao inazidi kuandamwa na pengo kubwa la wapulizaji wa ala za upepo.
“Hivi sasa ndani ya Msondo Ngoma kwenye ala ni kama tumebaki na Romario peke yake baada ya mwenzake, Ibrahim Mwinchande kufanyiwa upasuaji wa ngiri unaomlazimu kupumzika kazi kwa muda,” amesema Katundu.
Comments