MSANII anayefanya tasnia ya filamu nchini Salum Mpoyoka ambaye awali aliwahi kufanya vema
katika ujio wake wa filamu iliyoitwa 'Thank You loveness' ameanza maandali ya kufufua
namna mpya itakayovutia mashabiki wa saanaa.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana wakati msanii huyo alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari hizi ambapo alisema kuwa ameamua kuja kivingine baada ya kuangalia
mapungufu yaliyojitokeza kipindi cha nyuma katika sanaa ameamua kuja na kauli mbiu
ya Bongo Movie Mpya .
Alisema juhudi zake za sasa kupitia sanaa ni kufanya filamu zenye ubora wa mkubwa
kuzingatia mapungufu yalifanya sanaa hiyo isisonge mbele, huku akiwa amejipanga kutumia
wasanii chipukizi kusonga mbele.
"Filamu nitakazoanza kufanya kwa sasa zitajikita katika kuzingatia maadili ya kitanzania
na pia tutatumia weledi mkubwa katika kufanikisha ufanisi ili kuleta badiliko jipya katika
tasnia,"alisema Mpoyoka.
Mpoyoka alisema kuwa hilimsanii kujiunga na Bongo Movie Mpya anaweza kuwasiliana
kupitia instagram ambapo ataona neno new bongo movie amba kwenye akaunti za facebook
pamojana youtube.
Nyota huyo alicheza awali kabisa katika ujio wa Thank You loveness iliyowashirikisha nyota
wwngine katika uigizajiwa fiamu nchini kama msanii Mzee Chilo ,Mzee Magari, pamoja na Hashim
Kambi aliseweka wazi kuwa jana alianza uchukuaji wa picha akiwa na kundi la wasanii kibao
wanaoendelea kujitokeza kuunda umojawa wenye malengo ya maoni ya kurudisha watanzania
kurudisha kuanza upya kupenda vya nyumbani.
Comments