Rais wa Marekani, Donald Trump amewatoa hofu wafuasi wake baada ya
tetesi kuwa huenda mwanamke Mjasiriamali, Oprah Winfrey atajitupa kwenye
kinyang’anyiro cha urais wa nchi hiyo mwaka 2020.
Trump amesema anamfahamu sana Mwanamama huyo na ni moja ya watu ambao
huwa anafuatilia viindi vyake ingawaje huwa anaboreka na namna ya
uuliza maswali yake kwa wageni anaowaalika kwenye show zake huku
akipindisha baadhi ya ukweli wa mambo.
“Nimemtazama Oprah Winfrey mtu asiyekuwa madhubuti, ambaye
kwa upande mmoja namfahamu vizuri, nimekuwa nikimtazama akifanya
mahojiano na watu wengi kwa dakika 60. Maswali yake yamekuwa ya
upendeleo, yamekosa mwelekeo na amekuwa akipindisha ukweli, natumaini
Oprah anaweza akajitokeza na kugombea urais na nitamshinda kama
nilivyowafanyia wenzake,“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Mwishoni mwa mwaka jana Oprah wakati akitoa hotuba yake katika
ugawaji wa tuzo za Golden Globe aliushitua ulimwengu baada ya kutangaza
kuwa anaweza akagombea Urais wa Marekani mwaka 2020.
Hata hivyo, baadaye Oprah kupitia kipindi chake cha ‘Daytime Talk
Show’ alikuja kukanusha uvumi huo kwa kusema kuwa alitania tu ili
kunogesha hotuba kwani kazi hiyo haipo kwenye damu yake
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments