Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2018

CRA imepokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA). Nyimbo hizo ziliachiwa na wasanii katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii bila kupitishwa katika mamlaka husika kwaajili ya kuzikagua na baadaye kuiachia zipigwe. TCRA imesema nyimbo hizo zina maudhui kinyume na maadili na Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005, hivyo mamlaka hiyo imeviagiza vyombo vya habari kusitisha kuzicheza ngoma hizo.

Dkt.Philip Isdor Mpango :Takwimj sahihi zinasaidia kujua huduma zinazohitajika

Waziri wa fedha na mipango Dkt.Philip IsdorMpango amezindua rasmi ripoti ya uwasilishaji wa matokeo ya makisio ya idadi ya watu leo jijini Dar es salaam ambapo imeonekana kuwa Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na kubainika kuwa ifikapo mwaka 2021 idadi ya watu inakadiliwa kufikia milioni 77.5 Akiongea katika uzinduzi huo waziri Mpango amesema kuwa takwimu sahihi na kwa wakati sahihi zinasaidia kuboresha maisha wa watu na katika kupanga maendeleo ya muda mfupi, kati na muda mrefu ndani ya Taifa na kuongeza kuwa pia ni muhimu katika kupanga bajeti ya serikali kwani inarahisisha serikali kujua idadi ya nguvu Kazi waliyonayo. Pia amesema kuwa takwimj sahihi zinasaidia kujua huduma zinazohitajika na maeneo yanayohitaji huduma hizo na kusisitiza kuwa wingi wa watu siyo tatizo kwa nchi bali wingi wa ongezeko la watu unapozidi ongezeko la uchumi kwa nchi ndio huweza kutokea changamoto. Pia  waziri Mpango amesema kuwa kwa mjibu wa sensa ya ...

Yanga yapewa majina ya kikosi cha Township Rollers

Imebainik akuwa Uongozi wa Yanga, umepewa majina matatu ya nyota wanaokipiga kwenye kikosi cha Township Rollers ya Botswana ambao wanatakiwa kuwachunga ili wasiweze kuwaletea madhara watakapopambana katikati ya wiki ijayo. Jumatano ya wiki ijayo, Yanga inatarajiwa kucheza na timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Majina ya nyota hao watatu wanaokipiga kwenye kikosi cha Township Rollers ambayo inaongoza Ligi Kuu ya Botswana ni winga wa kulia Motsholetsi Sikele anayevaa jezi namba 28, kiungo wa kati Segolame Boy anayevaa jezi namba 11 (wote ni raia wa Botswana) na winga wa kushoto, Tshepo Matete, anayevaa jezi namba 18 ambaye ni raia wa Afrika Kusini. Akiwazungumzia nyota hao, Rashid Mandawa ambaye ni straika Mtanzania anayekipiga kwenye kikosi cha BDF XI ya nchini humo, alisema: “Wapo wachezaji wengi tishio kutokana na timu yenyewe jinsi ilivyo, lakini wale wanaocheza nafasi za mbele kama Bo...

Mbaroni kwa kumbaka Mtoto wa Miaka Minne

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Soli Mkanzabe (24), mkazi wa mtaa wa Nyegezi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa. “Inasemekana mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake. Mtoto alimfuata mtuhumiwa na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa alifanyia mtoto ukatili wa kumbaka na kumsababishia maumivu makali katika sehemu za siri huku mtuhumiwa akimwonya mtoto kuwa asiseme kwa mtu yeyote juu ya jambo hilo,” alisema DCP Msangi katik...

Huyu hapa Kimwana wa Jesse wa United

Wakati alipoifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili, mshabuliaji Jesse Lingard alishangilia katika namna ambayo mikono yake iliunda ishara ya herufi JL. Herufi J ilikuwa ikiwakilisha jina la kipenzi chake  Jena Frumes   wakati L iliwakilisha Lingard. Lingard alishangilia kwa staili hiyo ya kipekee kabla ya kwenda kuungana na swahiba wake Paul Pogba na kutengeneza ishara ya 'Wakanda Foreva' kutoka katika filamu inayoingisha dunia kwa hivi sasa " Black Panther". Katika kujibu mapigo ya mpenzi wake, kimwana  Jena Frumes naye akaingia dukani na kutengeneza kidani kilichokuwa na ishara ile ile ya ushangiliaji wa Lingard.

Beki wa klabu ya Simba Salim Mbode arejea mzigoni

Beki wa klabu ya Simba, Salim Mbode, jana amerejea rasmi mazoezini ndani ya kikosi hicho baada ya kupona majeraha ya goti. Mbonde alikosekana katika kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar FC, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba, zinzeleza kuwa Mbode ameanza mazoezi leo akiwa chini ya Mwalimu wa Viungo, Mohammed Hbibi, pamoja na Daktari wa timu, Yassin Gembe. Mbonde amerejea mazoezini ikiwa Simba inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC, ukaochezwa kesho Jumatatu jijini Dar es Salaam.

Nnyota Simba 'kamili gado' kuibutua Stand

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuhusu hali ya mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi kuwa yupo fiti licha ya kushindwa kuendelea na mchezo wa juzi Jumatatu walioibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC. Mganda huyo ameonekana kuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu, huku akifanikiwa kufunga mabao 16 ambayo yalifungwa na Simon Msuva msimu uliopita. Okwi alitolewa nje ya uwanja dakika ya 76  kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo. Simba waliweka taarifa kwenye ukurasa wao wa Istagram jana Jumanne ikieleza kwamba Okwi anaendelea vyema kutoka na majeraha aliyokuwa ameyapa wakati wakiisulubu Mbao FC. Ratiba iliyotangazwa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilieleza kwamba mchezo wa Simba na Stand United umerudishwa nyuma na utachezwa keshokutwa Ijumaa jijini Dar es Salaam. Lengo la kutoa nafasi hiyo ni kuwapa muda Simba kupata nafasi ya kufanya maandalizi kuelekea mechi yake ya kimataifa na Waarabu itakayopigwa Machi 9 Uwanja ...

WASICHANA 614,734 WENYE UMRI MIAKA 14 WATARAJI KUPEWA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZA

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(picha na mtandao) Na Hellena Matale Dar es salaam Serikali  imesema kuwa inatarajia kutoa chanjo kwa wasichana 614,734 wenye umri wa miaka 14 nchini ili kuwakinga na saratani ya shingo ya kizazi. Hayo yamebainishwa   na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  mapema leo  wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam. Amesema  kuwa kati ya wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti na vifo vitokanavyo na saratani kwa akina mama ni asilimia 50 ambapo chanzo ni saratani ya shingo ya kizazi na matiti. Aidha amesema amesema kutokana na mazingira ya upatikanaji wa chanjo hiyo na gharama kuwa kubwa, wataitoa kwa wasichana wenye miaka 14 waliozaliwa kati ya mwaka 2003 na 2004.    Naye Meneja wa...

Magazetini Leo

Dawa za kujichubua Ghana Zaonywa

WAJAWAZITO GHANA WAONYWA KUTUMIA DAWA ZA KUJICHUBUA Wanawake nchini Ghana wameonywa kutotumia dawa za kujichubua ilikubadilisha ngozi ya watoto kuwa nyeupe wakati bado wako tumboni. Wataalam wa afya wanasema dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika. Mamlaka ya Vyakula na Dawa Ghana (FDA) imesema utumiaji ya vidonge vya Glutathione ni hatari ikiongezea kuwa inataka " umma ifahamu kuwa hamna dawa zilizoruhusiwa na FDA aina ya vidonge vya kuchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni" Vitendo vinashamiri nchini Ghana, kwa mujibu wa FDA, mara nyingi vidonge vinaingizwa kinyemela ndani ya mizigo kwa viwango vikubwa kupitia viwanja vya ndege. Polisi na vikosi vya usalama wanafanya kazi pamoja kuwashika na kuwashtaki makampuni na watu binfsi watakaokuwa na vidonge visivyoruhusiwa.BBC

Nyota wa Paris St Germain Neymar hati hati kukosa mchezo dhidi ya Madrid, Barcelona wapatwa na pigo

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St Germain, Neymar Junior huenda akakosa mchezo wa klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid baada ya lkuumia vibaya jana usiku kwenye mchezo wa ligi nchini Ufaransa dhidi ya Marseille. Neymar Jr Neymar aliteguka kifundo cha mguu wa kulia kunako dakika ya 76 ya mchezo na kutoka nje huku akibubujikwa na machozi. Bado taarifa zaidi za kitabibu hazijatoka kutoka klabu hapo lakini huenda akakaa nje kuanzia wiki tatu, mwezi mmoja na kuendelea. Kwa hesabu hizo Neymar ana asilimia 60 kuukosa mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Machi 06 mwaka huu. Wakati PSG wakiwa njia panda juu ya mchezaji wao hali ipo tofauti kwa klabu ya Barcelona ambao hao tayari wameshapata pigo kwa kumkosa beki wao wa kulia, Nélson Semedo kwa mwezi mmoja baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Girona.

Mh. Zitto avamiwa na polisi

Mkutano wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya Defender. Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Chama hicho, imeeleza kuwa polisi baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi. Taarifa kwa waandishi MKUTANO wa ndani wa Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo,ndugu Zitto Kabwe uliokuwa unafanyika katika Kata ya Nambisi,wilayani Mbulu umevamiwa na Polisi wakiwa katika magari ya defender .Baada ya kuzungumza na Mwenyekiti wa Mkoa Manyara na kuelezwa kuwa kikao ni cha ndani hakihitaji Taarifa Polisi wameondoka na kuagiza diwani Wa kata huyo kuripoti kituo cha Polisi Abdallah Khamis Afisa Habari ACT Wazalendo 26/02/2018 Zitto yupo katika ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madi...

kikosi kitakachoanza leo na Mbao FC

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba, hii leo itaingia uwanjani kutupa karata yake  dhidi ya Mbao FC mchezo utakao pigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Kuelekea kwenye mchezo huo uliyokuwa muhimu zaidi kwa upande wa Simba SC katika kujihakikishia inajikusanyia pointi nyingi zaidi ili kuwa mbali na hasimu wake wa jadi Yanga SC, tayari wametaja kikosi kitakacho shuka dimbani leo hii. Simba SC wanaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 42 dhidi ya 37 ya Yanga SC inayoshika nafasi ya pili.