Paa la nyumba lililoezuliwa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Letisia Warioba akikabidhi mifuko ya unga wa ugali, kama ni moja ya msaada kwa waathirika wa mvua hizo.
Meneja wa Tanesco moa wa Iringa Donart Makingi akipita kati ya nguzo
zilizodondoshwa na mvua za upepo, katika eneo la Migori.
NA:
OLIVER RICHARD - IRINGA
MVUA
kubwa zilizoambatana na upepo mkali, zimevunja nyumba zaidi ya 50 na kuezua paa
katika Kata ya Migoli na Nyang’olo, katika Tarafa ya Isimani Wilaya ya Iringa,
na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi.
Wakizungumzia
tukio hilo, wananchi walisema mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa kumi
jioni, ambapo baadhi yao walikuwa katika mkutano wa mkuu wa mkoa, ambapo mvua
hiyo pia ilisambaratisha mkutano huo.
Maneno
Kalinga mkazi wa Nyang’olo alisema mvua hizo ziliambatana na upepo mkali na
hivyo kuezua paa la nyumba yake yote, na kudondosha kuta mbili za nyumba yake,
huku watoto waliokuwemo ndani ya nyumba wakipata madhara.
Kalinga
alisema kijana wake aitwaye Fadhili kalinga aliyekuwa amelala nadani ya nyumba
hiyo, aliangukiwa na ukuta na kuumizwa maeneo ya mgongo na kumsaidia kumuondoa
katika kifusi na kumuwahisha katika Zahanati ya Nyang’olo.
“Baada
ya kupiga kelele majira walikuja kumusaidia kijana wangu, na walipofanikiwa
kumtoa katika kifusi, tulimpeleka Zahanati kwa ajili ya kupata matibabu, na
hasara nyingine nilizozipata ni kubwa kwani vitu vyote vimelowa na kuharibika, “
Alisema Kalinga.
Estwina
Ngobola mkazi wa Migori alisema mali zake ziliharibiwa ikiwemo mifuko ya Sukari
kilo 25, unga wa ugali, unga wa ngano, godolo, huku vitanda na kochi vikivunjika
baada ya kuangukiwa na tofali
Alisema
“Niliingia chumbani ili nifunge dirisha upepo usiingie, kwani mvua ilikuwa na
upepo, nikawa ninahofu mji yataingilia dirishani, lakini nilipotaka kufunga
dirisha ulikuja upepo mkali nikaona nyumba inatikisika, nikakimbilia nje na
baadaye paa lote likatolewa na kutupwa pale, kuta zikadondoka, kama unavyoona
hivi,” Alisema Estwina.
Estwina
alisema kutokana na hali hiyo ameomba majirani wamuhifadhie vitu vyake, huku
yeye akiwa anaishi katika nyumba ya wageni, licha ya kutokuwa na fedha ya kulipa
kwani hana ndugu katika mkoa wa Iringa, kwani yeye ni mwenyeji wa Mbeya.
Lucia
Magidanga (98) mkazi wa Migori alisema hana mahala pa kuishi baada ya nyumba
yake kuezuliwa, huku akiwa hana msaada wowote wa kufanya ukatrabati wa nyumba
yake, kutokana na watoto wake wote kufariki.
Naye
Mwajuma Nzalamalenga alisema hasara aliyoipata kutokana na janga hilo ni kubwa
kwani mali zake zote zimeharibiwa vibaya, yakiwemo Magodoro, unga, Sukari,
Maharage, na nyumba ya mma yake ikiwa imeezuliwa yote.
Mwajuama
alisema hana mahala pa kuishi yeye na afamilia yake, na hata mvua ikianza tena
kunyesha haelewi hali halisi itakuwaje.
Aidha
mvua hizo pia zimeangusha nguzo 19 za Tanesco na hivyo eneo hilo kukosa nishati
ya umeme, ambapo meneja wa Tanesco mkoa wa Iringa Injinia Donart Makingi alisema
eneo hilo halina umeme kutokana na kuanguka kwa nguzo hizo.
Injinia
Makingi alisema tayari wanapeleka nguzo za umeme ili kurejesha nishati hiyo na
kuwa bado hajapata thamani halisi ya hasara itokanayo na janga hilo la mvua
zilizoambatana na upepo mkali.
Hatua
hiyo iliulazimu uongozi wa Mkoa kufika katika eneo la tukio kufanya tathimini ya
uharibifu uliotokea, huku waathjirika wakipatiwa baadhi ya misaada ya chakula
ili kuwasaidia wananchi hao.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Pudensiana Kisaka alisema wanafanya tathmini
ili kutambua kiwango cha hasara kilichopatikana kwa lengo la kuwasaidia wananchi
hao, huku akikabidhi Unga kilo 750 na Maharage kilo 300 kwa
waathirika.
Kisaka
aliwata wananchi hao kupanda miti kwa kiasi kikubwa msimu huu wa mvua ili
kuepukana na upepo mkali unaosababisha madhara makubwa kama ya kuezuliwa nyumba
zao na kupata hasara.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Letisia Warioba alisema mkoa kupitia mfuko wa maafa imeunda
kamati ya muda ya kutathimini madhara hayo ili kuweza kuwafidia wananchi
waliokumbwa na janga.Source Mjengwa.
Comments