Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi
ya The Kilimanjaro Band a.k.a Wananjenje,Waziri Ally akizungumza jambo
na Rais Kikwete Ikulu mapema leo walipokwenda kumpongeza kutokana moyo
wake mkunjufu aliounesha kwa kuwajali wasanii wa aina zote
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo
Desemba 21, 2012 amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi
pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kuwajali
wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii ambapo mwaka
huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.
Pichani kulia ni Rais Kikwete akipokea maneno ya sukurani kutoka kwa Mwanamuziki
Mkongwe wa bendi ya The Kilimanjaro Band a.k.a Wananjenje kwa niaba ya
wasanii wa filamu na wanamuziki waliofika Ikulu leo,jijini dar.
Mwanamuziki Mkongwe wa bendi ya
The Capital Mzee King Kikiii akipeana mkono na Rais Jakaya Kikwete huku
baadhi ya wanasanii wa filamu na muziki wakishuhudia tukio hilo mapema
leo,wakati wasanii hao walipokwenda kumpongeza Rais kwa kuwajali.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wasanii wa Filamu na wanamuziki wakongwe mapema leo Ikulu jijini Dar,walipokwenda kumpongeza Rais kwa kuwajali.PICHA NA IKULU.
Comments