Mshambulizi wa Manchester City
Kutoka Italia, Mario Balotellu, atafika mbele ya kamati maalum ya
shirikisho la mchezo wa soka nchini England siku ya Jumatano.
Balotelli anapinga uamuzi wa klabu yake ya
Manchester City ya kumpiga faini ya mshahara wake wa wiki mbili
kuhusiana na rekodi yake mbovu ya nidhamu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alikosa mechi 11 za ligi kuu na michuano ya ulaya msimu uliopita.
Balotelli alikata rufaa kuhusu aumuzi huo,
lakini kamati huru ya wanachama wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo
wakaifutilia mbali.
Balotteli anatarajiwa kufika mbele ya kikao
hicho binfasi, pamoja na wakili wake kutoka Italia na mwakilishi mmoja
wa chama cha wachezaji wa kulipwa, huku klabu ya manchester City
ikialishwa na mawakili wake.
Je Balotelli anastahili faini hiyo?
Faini hiyo ndicho kiwango cha juu zaidi
kuambatana na kandarasi ya wachezaji, lakini klabu ya Manchester City
imekataa kuzungumzia suala hilo na wanamatumaini makubwa kuwa jopo hilo
litafutilia mbali, rufaa hiyo.
Ni nadra sana kuona masuala ya ndani kati ya vilabu na wachezaji wao yalifika mbele ya kamati hiyo maalum.
Chama cha wachezaji wa soka wa kulipwa PFA,
kimekuwa kikitoa ushauri kwa Balotelli tangu mzozo huo kuanza na afisa
wake mkuu mtendaji Gordon Taylor, ameiambia BBC kuwa ''Tunajaribu kadri
ya uwezo wao kuzuia masuala kama hayo kufika mbele ya kamati hiyo ya FA,
lakini kwa kuwa mchezaji huyo na klabu yake hawajaafikiana''.
Klabu hiyo ilianzisha uchunguzi kuhusiana na
mchezaji huyo baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi yao dhidi ya
Arsenal Aprili mwaka huu.
Kwa ujumla, Belotelli amepewa kadi za njano tisa na tatu nyekundu.
Balotelli aliondolewa katika kipindi cha pili
wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester United ambapo walishindwa kwa
magoli 3-2 tarehe 9 mwezi huu, na kisha kuachwa nje ya kikosi cha
mabingwa hao watetezi wakati wa mechi yao dhidi ya Newcastle ambayo
walishinda kwa magoli 3-1.BBC.
Comments