Jocelyne Maro Miss East Africa 2012/2013 kutoka Tanzania akipunga mkono
kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo
lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya
Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka
lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye tmamani ya dola za kimarekani
30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji
kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu
mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda
Ayisha Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto na Miss
Burundi Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano
hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na warembo wenzake alioingia nao kwenye tano bora ya shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akiwa amepigwa na butwaa mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo jana usiku.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.
Warembo hawa ndiyo walioingia katika tano bora ya shindano la Miss East Africa.
Warembo hawa ndiyo walioingia katika kumi bora ya shindano la Miss East Africa.
Comments