Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
amesema wachezaji wa klabu hiyo hawapaswi kuabika kufuatia kuondplewa
kwao kwenye michuano ya kuwania kombe la ligi, na klabu ya Bradford
inayoshiriki ligi daraja ya pili.
Arsenal iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa kulazwa magoli 3-2 kupitia mikwaju ya penalti.
Baada
ya dakika 90 za kawaida kumalizika katika uwanja wa Croal Windows, timu
hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Akiongea na waandishi wa habaro baada ya mechi
hiyo Wenger alisema'' tulifanya kila kitu katika dakika mia moja
ishirini za mechi hiyo, na bila shaka timu ya Bradford ilicheza mchezo
mzuri na walistahili kushinda''
''Kwa kawaida ni jambo la aibu ikiwa hautacheza
kadri ya uwezo wako, nafikiria wachezaji wangu wamehuzunishwa na matokeo
hayo'' aliongeza Wenger.
Wenger alichagua kikosi kilichojumisha wachezaji
wake bora wakati wa mechi hiyo, lakini hawakufanikiwa kuandikisha
matokeo ya kuridhisha, na walihitaji bao dakika ya 88, bao lililofungwa
na Thomas Vermaelen ili kulazimisha mechi hiyo kwenda katika muda wa
ziada na hatimaye kuamiliwa kupitia mikwaju ya penalti.
Garry Thompson ndiye aliyeifungia Bradford bsao lake la kwaza katika kipindi cha kwanza.
Na kama desturi yake Wenger, alipuuzilia mbali
shutuma dhidi ya wachezaji wake , ambao wameshinda mechi moja tu kati ya
mechi sita walizocheza katika mashindano yote.Source. www.bbc.co.uk
Comments