MBUNGE wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila hilo la umma.
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Madini na Nishati alisema watu hao
ndio wanaoshirikiana kuihujumu Tanesco na kuliingiza taifa katika
hasara
Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo
baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa
kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali (CAG).
Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh
alisema uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni
kuikabidhi ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.
Mnyika aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa
walifanya uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na
kupendekeza kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza
masharti kwa sababu ya mgongano wa maslahi.
Mnyika alipendekeza vigogo hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Aliwataja watumishi wawili ambao walishindwa kutoa taarifa za ukiukaji
wa vigezo vya utoaji wa zabuni namba PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya
kampuni moja kati ya hizo mblii kupewa zabuni.
Alisema watendaji hao walichangia kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni
pamoja na kwamba haikuwa na fedha na kuiwezesha kupewa malipo ya
asilimia za ziada kinyume na mkataba.
Akapendekeza watendaji hao kuchuliliwa hatua za kinishamu. nMnyika
aliwataja watumishi wengine sita wa Tanesco ambao kwa pamoja walifanya
uamuzi uliosababisha kutolewa kwa mkataba namba PA/001/HQ/W/14 wa Machi
11,2010 kwa kampuni hiyo bila kuzingatia uwezo wa kitaalam, kifedha na
hivyo kukiuka sheria ya ununuzi wa umma.
Comments